Mambo ya Kuzingatia / Things to Observe
- Kufika shuleni kila siku: kufika saa 1:30 asubuhi (7:30 am), kutoka saa 10:00 jioni (4:00 pm).
- Kuvaa sare za shule kila awapo shuleni.
- Kuwa na vifaa vyote vya kujifunzia atakavyoagizwa na mwalimu.
- Kuzungumza lugha ya Kiingereza awapo katika maeneo yote ya shule.
Usafiri upo na ni wa uhakika katika pande zote za jiji. Karibu Mary's kwa huduma bora na za uhakika.
Sheria za Shule / School Rules
Mwanafunzi anapaswa / A pupil must:
- Kuwahi kufika shuleni, kufuata ratiba ya shule ipasavyo, kisha kurudi nyumbani mara baada ya ratiba ya shule kuisha.
- Kuhudhuria shule na vipindi vyote vya masomo.
- Kuwa msafi mwili na sare za shule wakati wote awapo shuleni.
- Kufanya kazi na mazoezi yote yanayotolewa na mwalimu.
- Kuwa na vifaa vyote muhimu vya masomo na kuvitunza ipasavyo.
- Kuepuka vitendo vyote visivyo vya kistaarabu, kiungwana na heshima, kama pombe, sigara n.k.
- Kuepuka matumizi ya lugha ya Kiswahili awapo katika mazingira ya shule, isipokuwa kipindi cha Kiswahili.
- Kutojihusisha na michezo yote inayovunja sheria za nchi, mfano kamari.
Ahadi ya Mwanafunzi / Pupil's Pledge
- Kwa kuwa nimejiunga na shule ya Mary's Pre and Primary, nitashiriki masomo kwa juhudi zangu zote ili kupata elimu yenye misingi imara.
- Nikiwa shuleni nitashirikiana na walimu na wanafunzi wenzangu wote katika kutafuta maarifa na ujuzi bora ili kuifanya shule kuwa bora kitaaluma.
- Adui yangu nikiwa shuleni ni mtu yeyote atakayesababisha kikwazo katika maendeleo yangu kitaaluma.
- Nitatumia elimu yangu si kwa manufaa yangu pekee bali kwa jamii inayonizunguka na taifa kwa ujumla.
Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.
Usaili wa Kujiunga / Entrance Interview
- Kumbuka kubandika picha za passport size kwenye fomu.
- Usaili unaanza saa 2:00 asubuhi (8:00 am) katika shule ya Mary's, Itezi.
- Usaili hufanyika kila Jumamosi na Jumatano na unahusu masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili.
- Wastani unaotakiwa: Daraja A (41–50) au A (81–100).
Our motto: Education our door to the future.